Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA MPANGO WA UWEZESHAJI WA FURSA ZA MIKOPO KWA MADEREVA BAJAJI NA BODABODA “NMB MASTABODA – MILIKI CHOMBO”


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akizungusha bango kuashiria uzinduzi wa mpango wa uwezeshaji wa mikopo kwa madereva Bajaji na Bodaboda ijulikanayo kwa NMB MASTABODA – MILIKI CHOMBO. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna (wa pili kutoka kulia). Kushoto ni Mwenyekiti wa Madereva Bodoboda Bw. Michael Massawe na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati Benki ya Nmb, Bw. Filbert Mponzi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akikabidhi funguo kwa dereva bodaboda ambaye amenufaika na mkopo wa NMB MASTABODA – MILIKI CHOMBO.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa amepakiwa kwenye pikipiki na mwendesha Bodaboda mara baada ya kuzindua rasmi fursa ya mikopo kwa madereva Bodaboda na Bajaji kupitia NMB MASTABODA – MILIKI CHOMBO.

Muonekano wa Pikipiki aina ya “Boxer” ambayo Benki ya NMB inatoa kama mkopo kwa madereva bodaboda kupitia NMB MASTABODA – MILIKI CHOMBO.

Baadhi ya Madereva Bajaji na Bodaboda walioshiriki katika hafla hiyo wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna akifafanua jambo kuhusu fursa ya mikopo inayotolewa na benki hiyo wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa “NMB MASTA BODA – MILIKI CHOMBO”, mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati Benki ya Nmb, Bw. Filbert Mponzi akieleza jambo wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Ubungo Plaza, Jijini Dar Es Salaam.