Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA RASMI BARAZA LA WAFANYAKAZI PSSSF


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughullikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amewataka wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kuhakikisha wanasimamia vyema yale yote ambayo wafanyakazi wanapaswa kuyafanya kwenye maeneo yao ya kazi.

Mheshimiwa Waziri Mhagama ameyasema hayo leo Februari 8, 2020 jijini Arusha wakati akizindua baraza la wafanyakazi PSSSF.

“Ninyi mnawakilisha kanda mbalimbali za Mfuko wetu, mnapaswa kuhakikisha hakuna uzembe katika utendaji wetu wa kazi, kuhakikisha wafanyakazi wanatimiza wajibu wao kulingana na malengo mliyojiwekea na pia kuwasilisha maoni ya wafanyakazi kwa menejiment ni nini wafanyakazi wanafiki tufanye ili kuboresha Mfuko wetu.” Alisema Mhe. Mhagama.

Alisema baraza la wafanyakazi ni kiungo muhimu kati ya Menejimenti na wafanyakazi katika kutengeneza chachu ya mfumo bora wa mawasiliano na majadiliano ili kujenga mazingira mazuri ya kutekeleza majukumu ya Mfuko.

“Kikao hiki ni utekelezaji wa agizo la Rais chini ya waraka namba moja wa mwaka 1970, waraka uliagiza kila taasisi ya serikali na binafsi kuhakikisha kwamba kuna mazingira wezeshi ya kusaidia uwepo wa majukwaa ya majadiliano baina ya waajiri na wafanyakazi ili kuboresha utendaji kazi kwenye eneo husika.” Alisema.

“Niwapongeze nini wafanyakazi na Menejimenti chini ya Mkurugenzi Mkuu, mmefanya kazi kubwa katika kutekeleza azma ya serikali na Rais wetu kuhakikisha kwamba uchumi wa taifa hili unakwenda kwa kasi kwa kuzingatia dira ya maendeleo tuliyo nayo hivi sasa ya kujenga uchumi wa viwanda.” Alisema na kuongeza……Ninyi pia ni wadau wakubwa katika uchumi huu wa viwanda, Mkurugenzi Mkuu ametoa taarifa nzuri ya miradi mbalimbali ya uwekezaji inayotekelezwa na Mfuko ikiwemo kiwanda cha bidhaa za ngozi hapo Karanga na hii ni heshima kwa taifa, ni heshima kwa Mfuko na heshima kwa watanzania na wafanyakzi wote wa PSSSF. “alisisitiza Mheshimiwa Waziri Mhagama.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Hosea Kashimba alisema, baraza hilo ndio lakwanza tangu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), liliundwa Juni 2019 ikiwa ni miezi minane tu tangu kuanzishwa kwa Mfuko.

Alisema katika kipindi kifupi tangu baraza lianzishwe limekuwa msada mkubwa kwa Mfuko katika kushauri menejiment kuhusu ufanisi wa kazi za Mfumo na kushauri mambo yanayohusu ustawi wa wafanyakazi wa Mfuko ambapo mambo mbalimbali yameendelea kuboreshwa.

“Kwa kipindi ambacho Mfuko umeanza kazi chini ya baraza hili kumekuwa na mafanikio kadhaa ikiwemo Mfuko kuwafikia wanachama wake wote kwa kufungua ofisi mikoa yote 28 ya Tanzania bara ikiwemo mikmoa mitatu ya kimkakati ya Ilala, Kinondoni na Temeke pamoja na Tanzania Zanzibar.” Alisema Bw. Kashimba.

Alisema Mfuko umekuwa ukitoa mafunzo kwa watumishi wake kuhusu mabadilko ya kimtazamo yaani culture change ili kujenga uwajibikaji wa pamoja.

Aidha Bw. Kashimba alisema ili kuhakikisha thamani ya fedha za michango ya wanachama inalindwa Mfuko umewekeza kwenye viwanda kama ambavyo kauli mbiu ya serikali ilivyo ambapo PSSSF imewekeza kwenye kiwanda cha kuchakata bidhaa za Ngozi Karanga kule Moshi, kiwanda cha kuchakata Tangawizi kule Mamba Miamba, Same na machinjio ya kisasa.