Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ndalichako akutana na kuzungumza na Uongozi wa UWAWABADA Jijini Dodoma


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekutana na kumanya mazungumzo na Uongozi wa Umoja wa Watu wenye Ulemavu waendesha Bajaji kutoka Mkoa wa Dar es Salaam (UWAWABADA) katika ofisi yake jijini Dodoma kwa lengo la kubadilishana mawazo na kujadiliana kwa pamoja changamoto mbalimbali zinazowakabili katika sekta hiyo.

Aidha, Katika kikao hicho viongozi hao na wajumbe wa UWAWABADA wametoa pongezi zao kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna anavyowapa kipaumbele Watu wenye Ulemavu. Pia wameishukuru Ofisi yake kwa namna inavyoshughulikia masuala mbalimbali yanayowakabili Watu wenye Ulemavu ili kuimarisha ustawi wa kundi hilo.