Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ndalichako ashiriki Mkutano wa 110 wa Kazi w Kimataifa nchini Uswisi


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameongoza ujumbe wa nchi katika Mkutano wa 110 wa Kazi wa Kimataifa leo Juni 7, 2022 Geneva, Uswisi.

Aidha, Waziri Ndalichako ameshiriki pia kikao cha kundi la Afrika ambapo ametoa salamu za nchi na kuwaalika nchi wanachama wa Afrika na Duniani kote kutembelea nchi ya Tanzania kwa lengo kujionea Vivutio vya kitalii na shughuli za ustawi wa wananchi zinazotekelezwa vizuri na Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.