Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

Waziri Sangu aitaka bodi ya PSSSF kuzalisha Ajira kwa Vijana


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Mhe. Deus Sangu (Mb) leo (Jumanne, Jan. 20, 2026) amekutana Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na kusisitiza umuhimu wa Mfuko kuwekeza katika miradi inayozalisha ajira kwa vijana wa kitanzania.

Katika mkutano huo uliofanyika katika Makao Makuu ya PSSSF jijini Dodoma, Mhe. Sangu amekumbusha kuwa kwa sasa Serikali inatekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo (DIRA 2025) ambayo, Pamoja na mambo mengine, inasisitiza uwekezaji katika miradi inayozalisha ajira na kuchochea Uchumi.


“Bodi ihakikishe mambo makubwa mawili katika utekelezaji wa miradi – kwanza kuzalisha ajira na pia ajira hizo ziwafikie vijana wa kitanzania kama DIRA 2050 na mipango ya Serikali inavyoelekeza,” amesema Waziri Sangu katika mkutano huo wake wa kwanza na Bodi ya Wadhamini ya PSSSF.

Katika mkutano huo, Menejimenti ya PSSSF nayo ilihudhuria ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Bw. Fortunatus Magambo.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSSSF Bi. Joyce Mapunjo, kwa niaba ya Bodi, alimuhakikishia Waziri Sangu kuwa utekelezaji wa majukumu ya Mfuko unaongozwa na Mpango Mkakati uliohuishwa kwa kuzingatia DIRA 20250 na miongozo ya Serikali.

“Tumepokea maelekezo na tutazingatia katika utekelezaji … nikuhakikishie kuwa tuna Mpango Mkakati mpya (2026/2027 - 2030/2031) unaozingatia mipango ya kitaifa na pia tunatumia utaalam na uzoefu wetu kuhakikisha malengo ya Mfuko yanatimia na unaendelea kuwa stahimilivu,” amesema Bi. Mapunjo ambaye ni Katibu Mkuu mstaafu aliyehudumu kwenye Wizara mbalimbali.

Mfuko wa PSSSF ulianzishwa mwaka 2018 kufuatia kuunganishwa kwa iliyokuwa Mifuko ya GEPF, LAPF, PSPF na PPF. Kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Mfuko, PSSSF ina majukumu manne ya kusajili wanachama, kukusanya michango, kuwekeza ili kutunza thamani ya fedha na kulipa mafao mbalimbali kwa wanachama wake.Waziri Sangu n