Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

Waziri Sangu ateta na Mkurugenzi Mkazi ILO


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) kwa nchi za Afrika Mashariki Caroline Mugalla, Februari 12, 2026 Ofisini kwake Jijini Dodoma.

Aidha, mazungumzo hayo yalilenga kujitambulisha rasmi kw

Mazungumzo hayo yalilenga kujitambulisha rasmi kwake na kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuhudumu katika Wizara hiyo.

Katika mazungumzo hayo, pande zote mbili zilikubaliana kuendeleza na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kwa lengo la kuboresha sekta ya Kazi, Ajira na Mahusiano nchini.

Pia, wameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa programu na miradi inayolenga kuongeza fursa za Ajira, kuimarisha mazungumzo ya kijamii na kuhakikisha viwango vya kazi vinazingatiwa kwa mujibu wa mikataba ya kimataifa.