Announcement
Matokeo ya Usaili kwa nafasi za Ajira ya Wauguzi Nchini Saudi Arabia
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU
TAARIFA KWA UMMA
MATOKEO YA USAILI KWA NAFASI ZA AJIRA YA WAUGUZI NCHINI SAUDI ARABIA
1. OWM - Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Kitengo cha Huduma za Ajira (TaESA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Dalba inapenda kuujulisha umma wa watanzania kuwa Wauguzi 240 kati ya Wauguzi 274 waliofanya usaili wa kazi za uuguzi nchini Saudi Arabia tarehe 3 - 4 Machi 2024 wamefaulu. Majina ya wauguzi waliofaulu yanapatikana kupitia www.kazi.go.tz.
2. Hatua inayofuata kwa Wauguzi waliofaulu usaili ni kupokea na kusaini barua za awali za kazi (Offer letters) na baadaye kufanya mtihani wa kitaaluma (Prometric Exams) utakaowawezesha wahusika kusajiliwa na Bodi ya Wauguzi nchini Saudi Arabia na kupata Leseni ya kufanya shughuli za uuguzi nchini humo kwa mujibu wa sheria.
3. Hivyo basi, Wauguzi waliofaulu waliopo jijini Dar es Salaam wanataarifiwa kufika Ofisi za TaESA tarehe 29 na 30 Mei 2024 kuanzia saa nane mchana kukutana na wawakilishi wa Wizara ya Afya ya Saudi Arabia (Kampuni ya Dalba) kwa ajili ya kusaini barua za awali za kazi (Offer letters) pamoja na kupokea maelekezo mengine muhimu kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa ajira. Wauguzi walio nje ya Dar es Salaam watapewa utaratibu wa namna ya kusaini barua za awali za kazi pamoja na maelekezo mengine.
4. Tunatumia fursa hii kuwapongeza wote waliojitokeza katika mchakato huu. Waombaji ambao hawakufanikiwa wanaweza kuomba tena mara nafasi zitapotangazwa.
5. Kwa maelezo zaidi wahusika wanaweza kuwasiliana na waratibu kupitia simu Na. 0735/39 221022 au barua pepe esu@taesa.go.tz.
Imetolewa na
KATIBU MKUU
OFISI YA WAZIRI MKUU
KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU
28/05/2024