Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

​BORESHENI MAZINGIRA YA KAZI KIAFYA – KATAMBI


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi ameuagiza uongozi wa Kiwanda cha Mbeya Cement kuhakikisha unatafuta mitambo ya kisasa kwa ajili ya kudhibiti vumbi la saruji inayozalishwa kiwandani hapo.

Mhe. Naibu Waziri Katambi ametoa agizo hilo Agosti 26, 2022 alipofanya ziara ya kushtukiza ya kukagua kiwanda hicho na kufuatilia utekelezaji wa sheria za kazi na masuala ya Usalama na Afya mahala pa kazi.

''Sijaridhishwa na hali niliyoikuta kimsingi eneo la uzalisha kuna vumbi ambalo limeshindwa kudhibitiwa na hivyo watumishi kuwa katika hatari kubwa ya kuugua magonjwa"

Mhe. Katambi alisisitiza kuwa usalama wa watu kazini ni muhimu na serikali itaendelea kusimamia sheria ili Watanzania wafanye kazi katika hali ya usalama sehemu za kazi.

”Katika kipindi cha mwezi mmoja nahitaji kuona mabadiliko ya namna ya kudhibiti vumbi ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa vifaa vya kujikinga na vumbi (barakoa)."

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Mbeya Cement, Khaledi Ghaleib alisema watahakikisha wanatekeleza maagizo hayo ya kuthibiti mifumo ya kusambaza kwa vumbi na kuwepo kwa vifaa vya kujikinga kwenye eneo la uzalishaji.