Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Dhamira ya Vyama vya Wafanyakazi Kuimarisha Umoja na Mshikamano: Mhe. Ridhiwani Kikwete


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete, amesisitiza umuhimu wa Vyama vya Wafanyakazi nchini katika kudumisha umoja na mshikamano kati ya wafanyakazi, viongozi wa vyama husika na serikali.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) uliofanyika Jijini Dodoma tarehe 8 Juni, 2025, Waziri Ridhiwani amesema uwepo wa vyama vya wafanyakazi umesaidia kuboresha utendaji kazi, kuongeza tija na ufanisi na kukuzs maendeleo ya taifa.

Waziri Ridhiwani pia amepongeza Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kwa mchango wake katika kuboresha sekta ya elimu na masuala ya kazi, akisema serikali inathamini ushirikiano wake kwenye utekelezaji wa sera na mipango.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali, huku Mgeni Rasmi akiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ambaye alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.