Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Kamati ya bunge yahimiza urithishaji ujuzi kwa wazawa


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii ameitaka Idara ya Kazi kuhakikisha inasimamia wageni walioajiriwa nchini kwenye miradi mbalimbali ikiwemo ya kimkakati kuhakikisha wanatekeleza mpango wa urithishaji ujuzi “Succession Plan” kwa wafanyakazi wazawa kama inavyoelekezwa kwenye Sheria ya kuratibu Ajira kwa Wageni.

Kamati hiyo imesema Mpango huo wa urithishaji ujuzi kwa wazawa utachagiza ushindani kwenye soko la ajira.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Fatma Towfiq Januari 17, 2024 Jijini Dodoma alipokuwa akipokea taarifa ya utekelezaji wa sheria ya kuratibu ajira kwa wageni, sura 346.

Kwa upande wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa Ofisi yake kupitia Idara ya Kazi itaendelea kutoa elimu kwa Waajiri na Wafanyakazi kuhusu sheria za kazi.

Naye, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ameeleza kuwa vibali ambavyo vinatolewa kwa wageni huzingatia faida mbalimbali ikiwemo za kiuchumi na kuzalisha fursa za ajira kwa wazawa.