Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Kamati ya Bunge yaipongeza WCF kwa kufanya kazi kwa weledi na kulipa fidia kwa wafanyakazi


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe. Rizick Lulida ameupongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi – WCF kwa kufanya kazi kwa weredi na kutoa fidia kwa wafanyakazi wanaopata ajali kazini.

Mhe. Lulida amebainisha hayo Oktoba 28, 2023 Jijini Dar es salaam wakati wa ziara ya kamati hiyo walipotembelea WCF kwa ajili ya kukaguza kazi zinazo fanywa na mfuko huo.

Aidha, ametoa rai kwa Mfuko huo kushiriki Mikutano ya Umoja wa Mataifa inayo husu watu wenye ulemavu ili kupata elimu na maazimio yatakayo wasaidia kutoa fidia stahiki kwa hao ikiwa ni pamoja na kujifunza namna ambavyo nchi nyingine zinavyo wafidia watu hao.

“Kuna sheria zinazoleta ukandamizi na ukakasi, ziwasilishwe kwenye kamati yetu ziweze kuboreshwa ili watu wapate haki zao, kuna watu wameumia lakini hawajui kama wanastahiki kulipwa kwa sababu sheria haikumwambia wala Ofisi, matokeo yake unakuta halipwi fidia yoyote. Tuko tatari kuzipeleka bungeni zifanyiwe marekebisho” amesema.

Akizungumza katika kikao hicho Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amesema katika kuhakikisha nguvu kazi ya Taifa inalindwa, mwajiri anawajibika kutoa michango kwa ajili ya wafanyakazi ili ikitokea madhira yatokanayo na kazi WCF itoe fidia.

Amesema miongoni mwa mafao yanayotolewa ni huduma ya matibabu, fidia ya ulemavu wa mudu mfupi na wa kudumu, malipo ya anayehudumia mgonjwa, huduma ya utengamao, malipo ya wategemezi na msaada wa mazishi.

Mhe, Katambi amesema Mfuko huo umeendelea kufanya vizuri kwa miaka sita mfurulizo na umekuwa wa kugwa Afrika Mashariki na kati.