Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

​Kamati ya Bunge yampongeza Rais Samia ukarabati na ujenzi wa vyuo vipya wenye ulemavu


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imempongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha fedha kwa ajili ya ukarabati wa vyuo vitano na ujenzi vyuo vipya vinne kwa Watu wenye Ulemavu.

Aidha, Kamati hiyo imesema vyuo hivyo vitatoa fursa kwa wenye Ulemavu kupata mafunzo ya stadi za kazi na huduma za marekebisho.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Fatma Tawfiq leo Januari 16, 2024 Jijini Dodoma wakati wa kikao cha kamati ikipokea taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa ukarabati na ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu.

Mhe. Tawfiq amesema Kamati hiyo inatambua mchango wa serikali katika kuthamini Watu wenye Ulemavu, hivyo itaendelea kuishauri serikali kuongeze bajeti kwa kundi hilo ili kukuza ustawi wao.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amesema Ofisi hiyo itahakikisha inasimamia ubora wa vyuo hivyo ili viweze kutoa mafunzo yaliyo kusudiwa kwa Watu wenye Ulemavu.