Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Kamati ya Bunge Yapitisha Maombi ya Bajeti Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA)


Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imepitisha maombi ya bajeti ya mwaka 2023/24 ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Kikao cha kamati hiyo kimefanyika leo Machi 23, 2023 bungeni na kuongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Fatuma Toufiq ambao CMA iliongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako.

Akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali, Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. Patrobas Katambi, amesema Tume hiyo imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na Idara ya Kazi ya Ofisi hiyo katika utatuzi wa migogoro ya kazi.

Awali, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu amesema dira ya Ofisi hiyo ni kuhakikisha inajenga jamii yenye mahusiano mema mahali pa kazi, nguvukazi shindani na maisha bora.

Katika taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya CMA kwa mwaka 2022/23, inaonesha Tume hiyo imesajili migogoro ya kikazi 12,570 ambapo migogoro 10,201 ilitatuliwa sawa na asilimia 81.2.