Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Kamati ya Bunge Yapongeza Utendaji Kazi wa OSHA


Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imepongeza utendaji kazi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) na kushauri kusimamia masuala ya usalama kazini ipasavyo kwenye maeneo ya miradi mikubwa.

Aidha, Kamati hiyo imeishauri serikali kuongeza bajeti ya usimamizi wa masuala ya usalama na afya ili kuuwezesha Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kuzuia ajali, magonjwa na uharibifu wa mali katika shughuli za uzalishaji hususan miradi mikubwa ya maendeleo jambo ambalo litaongeza kasi ya ukuaji wa uchumi nchini.

Ushauri huo umetolewa mara baada ya OSHA kuwasilisha randama ya bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 pamoja na taarifa ya muundo na majukumu yake mbele ya Kamati hiyo Bungeni Jijini Dodoma.Kamati ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii ndiyo inayoisimamia Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi chini yake ikiwemo OSHA kwasasa.

Hayo yameelezwa mara baada ya OSHA kuwasilisha randama ya bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 pamoja na taarifa ya muundo na majukumu yake mbele ya Kamati hiyo Bungeni Jijini Dodoma. Akizungumza, kwenye semina iliyoandaliwa na OSHA kwa wajumbe wa kamati hiyo Machi 22, 2023, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq, amepongeza OSHA kwa kutoa elimu ya utekelezaji wa majukumu yao kwa wajumbe na kuhimiza elimu itolewe zaidi kwa jamii ili kuitambua OSHA na kuhakikisha kunakuwa na usalama na afya kazini.

Naye, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Riziki Lulida, amesema wakala huo ni muhimu nchini katika kuimarisha afya za wafanyakazi kazini.

“Nashauri OSHA kupewa bajeti ya kutosha ili kufika maeneo yote muhimu ikiwamo mradi wa gesi asilia, bomba la mafuta,”amesema.

Katika kikao hicho ambacho OSHA iliongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako ameahidi kuzingatia ushauri wa wajumbe wa kamati hiyo.

Awali, Mtendaji Mkuu wa Wakala huo, Khadija Mwenda, amebainisha mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka miwili ya uongozi wa Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan ambayo ni ongezeko la kaguzi mahala pa kazi yaliyosajiliwa kutoka 4,336 hadi 11,353 sawa asilimia 276.

“Tumeongeza idadi ya kaguzi 104,203 hadi Machi, 2023 tumefikia 322,241 sawa na asilimia 132, inaonesha maeneo mengi ya kazi yamefikiwa na kushauriwa kuimarisha afya na usalama mahala a kazi,” amesema.