Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Kamati Yaridhia Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu


Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imepitisha Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Kikao cha kamati hiyo kimefanyika leo Machi 22, 2023 chini ya Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq ambapo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameiongoza Menejimenti ya Ofisi hiyo kuwasilisha mpango na bajeti ya ofisi hiyo.

Wajumbe wa Kamati hiyo walitoa maoni mbalimbali yaliyolenga kuboresha na kuwezesha utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi ili kuleta maendeleo na ustawi wa sekta ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu.

Aidha, Kamati hiyo imeishauri Serikali kuongeza wigo wa bajeti kwa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kutokana na mchango mkubwa ambao sekta hiyo inachagiza katika kukuza maendeleo ya Taifa.