Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Katibu Mkuu Maganga ataka WCF kuendelea kuzingatia ubora katika utoaji huduma


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi. Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu Mary Maganga ameutaka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi – WCF kuendelea kuzingatia ubora wa huduma inazotoa ili kuendana na ithibati ya utoaji wa huduma kwa viwango vya kimataifa.

Maganga ametoa agizo hilo Septemba 12, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati wakati wa hafla ya WCF kukabidhiwa Cheti cha Ithibati ya utoaji wa huduma bora kwa viwango vya kimataifa (ISO certification).

Aidha, amesema maboresho yanayofanywa na Mfuko huo yanapaswa kuzingatia mahitaji na matarajio ya wateja ili kuhakikisha wafanyakazi wanapatiwa fidia stahiki pale wanapopatwa na madhila yatokanayo na kazi zao.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa WCF Dkt. John Mduma amesema mafanikio waliyoyapata yamechangiwa na uwekezaji katika matumizi ya mifumo ya TEHAMA ili kuhakikisha wafanyakazi wanapatiwa fidia stahiki kwa wakati wanapopatwa na madhila yatokanayo na kazi.

“Tumewekeza katika matumizi ya Tehama, ambapo kwa sasa takribani asilimia tisini ya huduma za Mfuko zinapatikana kwa njia ya mtandao” amesema.

Awali akizungumza kwa niaba ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Viola Masako ameipongeza WCF kwa kukabidhiwa cheti cha ithibati ya utoaji wa huduma bora kwa viwango vya kimataifa.