Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

LESCO yafanya kikao cha kwanza Mwaka 2026/27


Baraza la Ushauri wa Masuala ya Kazi, Uchumi na Jamii (LESCO), kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, limefanya kikao chake cha kwanza kwa Mwaka wa Fedha 2026/27.

Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mheshimiwa Jaji Victoria Makani, na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya kazi, uchumi na jamii kwa lengo la kuendelea kuimarisha ushauri na mchango wa wadau katika maendeleo ya sekta hizo nchini.

Katika kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Best Western Hotel jijini Dodoma leo (01 Septemba 2026) wajumbe walipata fursa ya kujadili masuala ya kipaumbele katika sekta ya kazi, ikiwa ni pamoja na namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na wadau mbalimbali katika kushughulikia changamoto na kuboresha mazingira ya kazi nchini.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Bi. Zuhura Yunus, pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya kazi.

Baraza la LESCO linaendelea kuwa jukwaa muhimu la ushauri na majadiliano kuhusu masuala yanayogusa kazi, uchumi na jamii, kwa kuzingatia umuhimu wa ushirikishwaji wa wadau katika kuendeleza ustawi wa wananchi na maendeleo ya Taifa.