Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Maandalizi ya Mei Mosi Yamekamilika - Prof. Ndalichako


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema maandalizi ya Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi 2023 yamekamilika, ambapo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Prof. Ndalichako amesema hayo Aprili 30, 2023 alipokuwa akiwasilisha kwa Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa, taarifa ya maandalizi ya sherehe za Mei Mosi 2023 zitakazofanyika Kitaifa kesho Mei 1, 2023, katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Waziri Mkuu , Mhe.Kassim Majaliwa ameipongeza Kamati ya maandalizi hayo na kubainisha kuwa ameridhishwa na shughuli za Maandalizi zinazoendelea katika uwanja wa Jamhuri zitakapofanyika sherehe hizo.

Awali, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bi.Fatma Mwasa amesema kamati hiyo itahakikisha sherehe hizo zinafana.

Naye, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, Tumaini Nyamhokya, amesema kwa upande wa vyama vya wafanyakazi maandalizi yamekamilika na ni matarajio yao sherehe hizo zitafanyika kwa mafanikio.