Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

MATUKIO KATIKA PICHA OFISI YA WAZIRI MKUU BUNGENI DODOMA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo na Mbunge wa Mikumi Mhe. Joseph Haule mara baada ya kuhairishwa kwa mkutano wa Bunge unaoendelea Jijini Dodoma Aprili 9, 2019.

Sehemu ya Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia michango wa Wabunge mapema hii leo Bungeni Dodoma, katikati ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu Bi. Maimuna Tarishi, na mwenye tai nyekundu ni Katibu Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe wakati wa Bunge Jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde (wa kwanza kushoto) pamoja na Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile (mwenye tai ya blue) wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Andrew Massawe (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) mwenye tai nyekundu na Bi. Maimuna Tarishi (Bunge na Waziri Mkuu) nje ya Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

Makatibu Wakuu Ofisi ya Waziri Mkuu wakiteta jambo mara baada ya kuhairishwa kwa vikao vya bunge vinavyoendelea Jijini Dodoma Aprili 09, 2019, kulia ni Bw. Andrew Massawe anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na kushoto ni Bi. Maimuna Tarishi (Bunge na Waziri Mkuu)