Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mfuko Wa Self wapongezwa kwa kutoa msaada wa Vitanda na Magodoro Yenye Thamani Ya Tsh. Milioni 29


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi ameupongeza Mfuko wa SELF kwa kutoa msaada wa magodoro 80 na vitanda 40 vyenye thamani ya Tsh. milioni 29.390,600 kwa chuo cha ufundi cha walemavu Yombo Kiwalani jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo Naibu Waziri Katambi alisema kwamba taasisi hiyo imefanya jambo jema kwa kusaidia chuo hicho kikongwe cha walemavu nchini kupata vifaa hivyo kwa ajili ya malazi ya wanafunzi.

Alisema serikali ya awamu ya sita itaendelea kuborsha sera na kubadilisha sheria ili kuhakikisha haki za walemavu nchini zinalindwa kikamilifu.

“Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imetenga Tsh. bilioni 8 ili kuboresha vyuo vyote vya watu wenye ulemavu hapa nchini,”. Msaada huo uliotolewa na mfuko huo unaunga jitihada za serikali katika kupunguza adha ya vifaa vya malazi kwa wanafunzi wa chuo hicho, aliongeza kusema.

Alifafanua kwamba vyuo vya ufundi vya watu wenye ulemavu vipo sita hapa nchini kikiwemo cha Tanga, Tabora, Dar es Salaam, Mtwara, Mwanza na Zanzibara.

Alisema serikali itaendelea kuboresha ,miundombinu ya chuo hicho ili kila mtoto mwenye ulemavu aweze kupata elimu ya ufundi stadi na kusema ni muhimu kwa watu wenye ulemavu hapa nchini kutungiwa sheria zinazowalinda kwa ustawi wao.

“Tunajua kwamba watu wenye ulemavu wapo katia makundi maalum na wanahitaji kupata mafunzo ya ufundi stadi kulingana na makundi yao,”. Serikali iliamua kuanzisha vyuo hivyo ili kila mtanzania nashiriki katika shughuli za kijamii na kiuchumi na kujenga taifa.

Alisema anawashukuru watendaji wa mfuko huo kwa kusaidia vitanda na magodoro wanafunzi wenye ulemavu na kuzitaka taasisi na kampuni mbalimbali kuiga mfano huo.

Kwa upande wake Afisa Mtndaji Mkuu wa Mfuko wa Self, Bw.Mudith Cheyo alisema mfuko huo ulianzishwa September 2014 kwa lengo la kutekeleza sera ya serikali ya uwezeshaji wanachi kiuchumi.

“Leo tumekuja kutoa msadaa kwa chuo hiki cha watu wenye ulemavu ili kuunga mkono serikali katika kusaidia watu wenye ulemavu,” Hiyo itasaidia kupunguza adha ya uhaba wa vifaa vya malazi na pia wajisikie tunawapenda aliongeza kusema Bw, Cheyo.

Alisema pia mfuko wao unatoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wananchi wenye kipato cha chini hususani vijijini na kwamba hadi kufikia Desember 2021 wametoa mikopo yenye thamani ya Tsh. 257.0 bilioni kwa wakopaji, 187, 731 pamoja na kuendelea kutoa mikopo kwenye taasisi mbalimbali,

Alisema taasi hiyo imeendelea kutoa huduma bora kwa watanzania kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa watu wenye kipato cha chini, kati na wajasiriamali ambao hasa wako vijijijini.

Cheyo aliendelea kufafanua kwamba mfuko utaendelea kutoa huduma zake ili kuchangia kuleta mapinduzi ya uchumi hapa nchini.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Mariam Chillangwa alisema chuo kinatoa mafunzo ya ufundi stadi kama vile umeme wa majumbani, useremara, ushonaji, utengenezaji wa makabati na upishi,

Pia chuo kinawafundisha wanafunzi stadi za maisha ili waweze kukabiliana na changamoto na maisha wanapomaliza masomo yao chuoni, aliongeza kusema Bi. Chillangwa.

Mkuu huyo wa chuo aliomba wadau mbalimbali waendelee kusaidia chuo hicho ili kiweze kukidhi mahitaji ya miundombinu kwa wanafunzi wake.