Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mhe. Katambi atoa maelekezo sita kwa NSSF na PSSSF


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi ametoa maagizo sita kwa Wakurugenzi Wakuu wa Mifuko ya Pensheni yanayolenga kumaliza malalamiko ya wanachama wa mifuko hiyo.

Aidha, ametoa onyo kwa waajiri kuhakikisha wanawasilisha michango na taarifa za kustaafu za watumishi wao kwa wakati.

Mhe. Katambi ameyasema hayo Juni 20, 2023 jijini Dodoma alipokuwa akizungumzia kuhusu changamoto wanazokutana nazo baadhi ya wanachama na wastaafu wanapofuatilia mafao kwenye mifuko ya pensheni.

Vile vile, ameelekeza waajiri wote kuhakikisha wanalipa na kuwasilisha madeni ya michango ya watumishi wao kila mwezi, kila Meneja wa Mkoa awasilishe majina ya waajiiri sugu wanaodaiwa michango ya wafanyakazi wao ndani ya siku saba kuanzia leo na kusiwe na malalamiko ya wanachama kwenye maeneo yao.

Pia, ameagiza kila Mfuko uhakikishe mwanachama analipwa mafao ndani ya siku 60 za kisheria, kuwasikiliza na kutoa elimu kuhusu taarifa za wanachama na watumishi wa mifuko watapandishwa vyeo kwa kuzingatia utendaji na uwajibikaji katika kuwahudumia wanachama.

Kwa upande mwengine, Mhe. Katambi ametoa namba za mawasiliano ili wananchi waweze kupata ufafanuzi zaidi kwa kupiga simu ya bure Mfuko wa PSSSF ni 0800110040 na NSSF ni 0800116773.