Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

​Mhe. Katambi azindua Taasisi ya NGUVUMOJA YOUTH POWER FOUNDATION


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amezindua rasmi Taasisi ya NGUVUMOJA YOUTH POWER FOUNDATION leo Juni 8, 2024 Jijini Dodoma.

Taasisi hiyo ina Lengo la kuongeza wigo kwa vijana kujiajiri na kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira nchini.

Aidha, Katambi amesema Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani ameendelea kuwainua vijana kiuchumi kwa kutoa pesa kupitia Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora – BBT, kutoa mafunzo ya uanagenzi awamu ya sita kwa Vijana 6,000, kuanzishwa kwa programu ya Ukuzaji Ujuzi na kufanya maboresho ya Mwongozo wa Utoaji Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF).

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema Serikali imeboresha Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023 ambapo sasa inatoa upendeleo kwa makundi ya vijana, wanawake, Wenye Ulemavu na Wazee kushiriki katika mchakato wa manunuzi ya Umma ambapo hadi sasa, Kampuni zaidi ya 118 za vijana zimeundwa na kunufaika na 30% ya sheria ya manunuzi ya umma.

Naye, Mkurugenzi wa Taasisi ya NGUVUMOJA YOUTH POWER FOUNDATION Anold Nyato amesema Taasisi hiyo itakuwa na Vijana wenye umri wa Miaka 18-35 wenye Mawazo bunifu ya biashara.

“Taasisi hiyo itajihusisha na vijana kuanzia umri wa miaka 18 hadi 35 bila kujali wapo mtaani au bado wana