Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

​Mhe. Katambi: Baraza la watu wenye ulemavu linatekeleza majukumu yake


Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amesema Baraza la ushauri la watu wenye ulemavu lilishaundwa na Rais kwa mujibu wa sheria na linatekeleza majukumu yake ipasavyo.

Mhe.Katambi ameyasema hayo bungeni Januari 30, 2024 alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Vitimaalum, Mhe. Khadija Taya ambaye ametaka kujua lini mara ya mwisho baraza hilo limekaa kikao chake.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Katambi amesema mara ya mwisho baraza hilo limekaa kikao chake Desemba 2023 na miongoni wa kazi zilizofanyika ni kushauri marekebisho sera ya watu wenye ulemavu ambayo imedumu kwa muda mrefu na maandalizi ya kuboresha Sheria ya watu wenye ulemavu yam waka 2010.

Ametaja majukumu ya baraza hilo ni kumshauri Waziri anayehusika na watu wenye ulemavu juu ya utekelezaji wa sheria hiyo hususani katika utoaji wa haki za usawa baina ya wanawake na wanaume wenye ulemavu, afya, marekebisho, elimu, ajira, miundo mbinu, mafunzo ya ufundi stadi na haki nyingine.