Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mhe. Ummy Nderiananga atembelea Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Maonesho ya Nanenane


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga ametembelea banda jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake katika maonesho ya kilimo ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma Agosti 04, 2025.

Katika Banda hilo Mhe. Nderiananga ameona mifumo mbalimbali ikiwemo mfumo wa Taarifa za Watu wenye Ulemavu (Persons with Disabilities Management Information System -PID-MIS) ambalo ni jukwaa la kidigitali linalotumika nchini Tanzania kwa lengo la kukusanya, kuhifadhi, kuchambua na kutoa taarifa sahihi zinazohusu Watu wenye Ulemavu .

Aidha, amewapongeza watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zake kwa kuendelea kutoa elimu kwa umma na wadau katika maonesho hayo.

Katika hatua nyingine, Mhe. Nderiananga amehamasisha wananchi kuendelea kutembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu ili kupata uelewa wa shughuli zinazotekelezwa na ofisi hiyo.

Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni: “Chagua Viongozi Bora kwa maendeleo endeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025”