Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mifuko ya Hifadhi ya Jamii yahamasishwa kutoa elimu kwa wanachama


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeitaka Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutoa elimu mara kwa mara ili kuongeza uelewa kwa wanachama.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq (Mb) ametoa wito huo leo Februari 7, 2024 alipokuwa akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo kuhusu shughuli za kamati kwa mwaka 2023.

Vile vile, Kamati hiyo imetaka Mfuko wa PSSSF na NSSF kuchukua hatua za kisheria kwa waajiri wanaowasilisha michango iliyo na kiwango chini ya mishahara halisi kwa watumishi.