News
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye aongoza zoezi la Usafi Makazi wa Wazee Kibirizi
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye ameongoza zoezi la usafi katika Makazi ya Wazee wasiojiweza Kibirizi mkoani Kigoma ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Kukuza uelewa kuhusu Ualbino yatakayofanyika Juni 13, 2025.
Akizungumza leo Juni 11, 2025 baada ya zoezi hilo, Mhe. Andengenye ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo na Mikoa jirani kujitokeza kwa wingi katika siku hiyo ili kupata elimu kuhusu masuala ya watu wenye Ualbino.
Naye kiongozi wa Chama cha Watu Wenye Ualbino (TAS) Godson Mollel amesema kuwa kama chama wamejipanga vyema kutumia maadhimisho hayo kutoa elimu kwenye jamii ili kupata uelewa kuhusu watu wenye Ualbino.
Katika hatua nyingine Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imeupongeza uongozi wa Mkoa kwa maandalizi mazuri ya kuelekea maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Kukuza uelewa kuhusu Ualbino.
Aidha Afisa Ustawi wa Jamii Mfawidhi ambae pia ni msimamizi wa kituo cha Makazi ya Wazee wasiojiweza Kibirizi Binura Joshua ameshukuru wadau wote kwa kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita ikwa kuwakumbuka wazee wa kituo hicho chenye idadi ya wazee 29 wakike 12 na wakiume 17.