Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Naibu Waziri Katambi ahimiza Sehemu za Kazi kuwa na Mipango ya Kuboresha Afya na Usalama Mahali Pa Kazi


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amezihimiza Taasisi zinazoshiriki Maonesho ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya mahali pa kazi kuwa na mipango katika sehemu zao za kazi ya kuboresha masuala ya Afya na usalama mahali pa kazi .

Mhe. Katambi amebainisha hayo Aprili 30, 2023 alipotembelea viwanja vya Tumbaku Mkoani Morogoro yanapofanyika maonesho hayo ambapo alitembelea mabanda ya washiriki wa maonesho hayo..

Amesema Taasisi zilizoshiriki maonesho hayo tayari zimefanikiwa kuwa na mipango ya uboreshaji na udhibiti wa madhara yatokanayo na kazi kwa wafanyakazi hivyo amewahimiza elimu ya afya na usalama mahali pa kazi iendelee kutolewa kwa kiwango kikubwa ili kuboresha mazingira ya kazi.

Amebainisha kuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameweka jitihada za kuhakikisha uwekezaji nchini unakua, kuongeza fursa za kiuchumi na ajira ili kuwaletea maendeleo watanzania hivyo hakuna budi usalama na Afya mahali pa kazi kuimarishwa.

Mhe. Katambia amempongeza Mkurugenzi wa Wakala wa Usalama Mahali pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda kwa uratibu na usimamizi mzuri wa masuala ya afya na usalama mahala pa kazi nchini.