Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Ndejembi awataka Wakuu wa Mikoa kuanzisha operesheni za ulinzi kwa Watu Wenye Ualbino


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka Wakuu wa Mikoa nchini kuanzisha Operesheni maalum za ulinzi kwa Watu Wenye Ualbino.

Aidha, amesema Operesheni hizo zihusishe vikosi vya Usalama ili kuhakikisha ulinzi wa watu hao dhidi ya mashambulizi na vitisho.

Mhe. Ndejembi ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao kazi na Wakuu wa Mikoa wote nchini kilichofanyika kwa njia ya mtandao.

“Washirikisheni na kuwahimiza viongozi wa kimila kushiriki kikamilifu katika kukemea na kupinga mauaji ya watu wenye Ualbino kwa kuwa viongozi hawa wana nafasi kubwa na wamekuwa nguzo muhimu katika jamii” amesema.