Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Ndejembi: Serikali inaendelea kutoa Mikopo 10%


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe Deogratius Ndejembi amesema Serikali inaendelea na utaratibu wake wa kutoa mikopo ya asilimia 10 kupitia Halmashauri pamoja na mikopo ya vijana kupitia mfuko wa vijana unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi Vijana Ajira na wenye Ulemavu.

Mhe Ndejembi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya NMB JIWEKEE jijini Dar es Salaam leo.

Mhe Ndejembi amesema iko mikakati ambayo serikali imeendelea kufanya ili kuongeza kipato kwa wananchi wake ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo mbalimbali yanayoratibiwa na Wizara kupitia Vyuo vya Ufundi Stadi VETA ili kuwapa ujuzi utakaowawezesha kujiajiri.

“ Serikali inaendelea kutoa wito kwa Taasisi za Kifedha kuendelea kutoa elimu kwa wananchi hasa vijana ili kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba itakayowasaidia mbeleni. Niwapongeze Benki ya NMB kwa kuja na wazo la NMB Jiwekee ambalo linawagusa wananchi wote walio nje ya mfumo rasmi wa ajira ili kujiwekea akiba,” Amesema Mhe Ndejembi.