Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Ofisi ya Waziri Mkuu kazi yapongezwa kutoa mafunzo ya ukuzaji ujuzi


Katibu Tawala Mkoa wa Geita Bw. Mohammed Gombati ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kutoa mafunzo ya kukuza ujuzi kwa wachimbaji wadogo wa Madini wa Mkoa wa Geita.

Bw. Gombati amebainisha hayo leo Juni 25, 2025 mkoani humo wakati akifungua Mafunzo ya ukuzaji Ujuzi kwa wachimbaji hao, ambapo amesema jumla ya wachimbaji 600 wa Mkoa wa Geita, Wilaya ya Mbogwe na Chunya watapatiwa mafunzo ya Ukuzaji ujuzi.

Aidha, amesema hadi sasa Ofisi hiyo, kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi imetoa mafunzo kwa kwa Wafanyakazi 17, 352 wanaofanya kazi katika maeneo mbalimbali nchini,

Awali akizungumza Kaimu Mkurugenzi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi hiyo, Bi. Alana Nchimbi amesema Programu hiyo imejikita katika mafunzo ya Uanagenzi (Apprenticeshiptraining), Mafunzo ya kurasimisha ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa ujuzi, Mafunzo kwa vitendo mahali pa kazi kwa Wahitimu (Internship training) na Mafunzo ya kukuza ujuzi kwa walio makazini.

Mafunzo hayo yanayotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, lengo ni kuhakikisha nguvukazi ya Taifa inapata ujuzi stahiki ili iweze kujiajiri au kuajiriwa, sambamba na kupunguza nguvukazi isiyo na ujuzi stahiki unaohitajika katika soko la Ajira.