Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Ofisi ya Waziri Mkuu Yashiriki Wiki ya Utumishi wa Umma


Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo zinashiriki kikamilifu katika Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.

Taasisi hizo zinazoshiriki ni Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).

Aidha, Kupitia maonesho hayo wananchi kutoka maeneo mbalimbali wametembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu kwa lengo la kupata fursa ya kujifunza kuhusu shughuli ziazoteklezwa na ofisi hiyo. Maadhimisho hayo yamefunguliwa rasmi leo, tarehe 17 Juni, 2025 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ambapo Wiki ya Utumishi wa Umma ni jukwaa muhimu la kuonesha uwajibikaji wa watumishi wa umma na kuboresha mahusiano kati ya Serikali na wananchi.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu 2025 ni "Himiza matumizi ya mifumo ya kidigiti ili kuongeza upatikanaji wa taarifa na kuchagiza uwajibikaji"