Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

​Ofisi ya Waziri Mkuu yawapiga msasa wastaafu watarajiwa


Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Kitengo cha Ukuzaji Tija kimetoa mafunzo kwa Watumishi wa sekta ya umma na sekta binafsi ambao wanatarajia kustaafu ili waweze kumudu maisha yao.

Akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo hayo leo Juni 30, 2023 mkoani Morogoro, Mkurugenzi wa Ukuzaji Tija, Bw. Yohana Madadi amewasihi watumishi hao kujenga utamaduni wa nidhamu katika matumizi ya rasilimali ikiwemo fedha watakazopata kama kiinua mgongo.


Ameongeza kuwa, masomo yaliyotolewa na wawezeshaji yatawasadia kuwawezesha kujipanga baada ya kustaafu, kuwekeza kwenye miradi yenye tija ikiwemo shughuli za ujasiliamali, ufugaji, kilimo na uzalishaji.

“Nidhamu ya maisha baada ya kustaafu ni muhimu sana hivyo, mafunzo haya tunayatoa ili kumuandaa mfanyakazi na maisha baada ya kustaafu,” amesema.

Kwa upande wa aliekuwa Mwenyekiti wa Mafunzo hayo Bw. Sagana Machogu kutoka Tanzania Commercial Bank (TCB) amesema mafunzo hayo yamekuwa ni muhimu kwao na wameahidi kufanyia kazi mafunzo waliyopatiwa.

Naye Mshiriki wa mafunzo hayo, Bi. Jennifer Msalya kutoka Taasisi ya Hifadhi ya Bahari na maeneo Tengefu, ameishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuwawezesha mafunzo hayo na kushauri kitengo hicho kuongea na waajiri na kuwapa msisitizo wa mafunzo hayo kutolewa kwa wafanyakazi kabla ya kustaafu.

Mafunzo hayo yametolewa kwa watumishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bodi ya Ununuzi na Ugavi, Tume ya Matumizi ya Ardhi, Taasisi ya Hifadhi za Bahari na maeneo Tengefu, Shirika la Maendeleo ya Petroli na Benki ya Biashara (TCB).

Kitengo cha Ukuzaji Tija ni kinatekeleza majukumu yanayolenga kukuza tija na ubunifu kwa maendeleo na ukuaji wa uchumi.