Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Prof. Katundu atoa wito kwa wadau kushiriki utekelezaji wa vipaumbele vya Ofisi ya Waziri Mkuu



Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Watu wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu ametoa wito kwa wadau wa maendeleo kushirikiana na Ofisi hiyo katika kutekeleza vipaumbele vya Ofisi hiyo ili kuweza kufanikisha wa mipango, miradi na mikakati itakayowezesha uwepo wa Jamii yenye mahusiano mema mahali pa kazi, nguvu kazi shindani na Maisha bora.

Prof. Katundu amebainisha hayo Juni 30, 2023 Jijini Dar es Salaam kwenye kikao cha wadau wa maendeleo wa Ofisi hiyo kilicholenga kuwaelezea vipaumbele vya Ofisi hiyo katika kuelekea katika utekelezaji wa bajeti ya mwak 2023/2024.

Vipaumbele hivyo ni upatikanaji wa fursa za ajira, kuboresha maslahi na mazingira ya wafanyakazi, kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa Watu Wenye Ulemavu, kusimamia utekelezaji wa Sheria za Kazi.

Aidha, amesema vipaumbele vingine ni kuwa na programu zinazolenga kuweka mazingira ya vijana kupata mitaji, elimu ya ujasiriamali na kuongeza wigo wa matumizi ya Teknolojia mpya za kidigitali ili kuongeza ufanisi wa kurahisisha upatikanaji wa huduma za Serikali.

Amesema kwa mujibu wa hati Idhini iliyotolewa mwezi Januari, 2022, Ofisi hiyo imepewa jukumu la kuratibu masuala yanayohusu Kazi, Vijana, Ajira, Watu Wenye Ulemavu nchini, Hifadhi ya Jamii na Kukuza Majadiliano ya pamoja Mahali pa Kazi.

Sambamba na hayo, amesema Majukumu ya Ofisi hiyo yanatekelezwa kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa mwaka 2021/22- 2025/26, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2020 -2025, Mpango wa tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP III) 2021/22 - 2025/26 na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020.