Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Katibu Mkuu Prof. Katundu: Mikopo ya Sh. Bil. 3 imetolewa kuwezesha miradi ya Vijana


Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu amesema katika mwaka wa fedha 2022/23, hadi kufikia Agosti 2023/24, kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana unaoratibiwa na ofisi hiyo, Sh. bilioni 3.2 zimekopeshwa kwa vijana kutekeleza miradi 149.

Akifungua kongamano la kitaifa la vijana katika kuelekea siku ya kimataifa ya vijana Agosti 11, 2023 jijini Dodoma, Prof. Katundu amesema miradi hiyo ni ya kwenye sekta ya kilimo, viwanda, usafirishaji na biashara.

Prof.Katundu, amefafanua kuwa kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 idadi ya vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15-35 ni asilimia 34.5, hivyo vijana wanatakiwa kujengewa uwezo wa kiuchumi.

Naye, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania, Zlatan Milisic, amesema kuna umuhimu wa vijana kujengewa uwezo wa kiuchumi ili waweza kuchangia katika kuinua pato la taifa.