Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Prof. Ndalichako asisitiza mambo matatu utafiti watu wenye kufanya kazi 2024


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ametoa wito kwa viongozi wa Serikali katika ngazi za utawala kutoa ushirikiano kwa wadadisi na wasimamizi wa Utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2024.

Prof. Ndalichako ametoa wito huo Januari 19, 2024 Mkoani Morogoro wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wadadisi na wasimamizi wa utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2024.

Pia, ametoa rai kwa wananchi katika maeneo yaliyochaguliwa kwenye utafiti huo kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kujibu maswali watakayoulizwa na kutoa taarifa sahihi ambazo zitakuwa siri na zitatumika kwa shughuli za kitakwimu pekee.

Kwa upande mwengine, amewahakikishia wananchi kuwa shughuli zao za kiuchumi na kijamii hazitasimamishwa na zoezi la Utafiti huu kwa kuwa wadadisi watakusanya takwimu za Utafiti wakati shughuli zingine zikiendelea kama kawaida.

Prof. Ndalichako ameongeza kuwa, matokeo ya utafiti huo yatasaidia kupima utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2025 kwa Tanzania Bara na yatatatumika kupima utekelezaji wa Programu mbalimbali za kupima ukuzaji ujuzi na uzalishaji wa fursa za Ajira.