Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Prof. Ndalichako awataka maafisa kazi kuendelea kusimamia Haki za Wafanyakazi nchini


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amewataka Maafisa kazi wafawidhi nchini kuhakikisha wanasimamia haki za wafanyakazi nchini.

Prof. Ndalichako amebainisha hayo leo Juni 27, 2023 wakati akizungumza na Maafisa kazi Wafawidhi wa Mikoa kwenye mafunzo yaliyoratibiwa na ofisi hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO), jijini Arusha.


Aidha, Prof. Ndalichako amesema kufanya hivyo kutawezesha uwepo wa kazi zenye staha na usimamizi mzuri wa haki za wafanyakazi, ikiwa ni dhamira ya Serikali anayoiongoza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuendelea kuimarisha maslahi ya wafanyakazi nchini.

Kwa upande mwengine Katibu Mkuu - Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu amewasisitiza maafisa hao kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma zao, kuwa wabunifu, waadilifu na kufanya kazi kwa umoja.

Naye, Mkurugenzi Mkazi wa ILO Afrika Mashariki, Jealous Chirove amesema watendelea kushirikiana na Serikali na kuunga mkono juhudi za zake ili maeneo ya kazi yaendelee zingatia masuala ya haki na usawa kwa wafanyakazi.