Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA SHEREHE ZA MWENGE WA UHURU, MKOANI LINDI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameongoza sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wiki ya Vijana Kitaifa na Kumbukizi ya ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Wakati wa Maadhimisho hayo Rais Dkt. John Magufuli aliiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi kwa miradi 107 yenye thamani ya shilingi Bilioni 90.28 iliyobainika wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu (2019) kuwa na dosari mbalimbali zikiwemo kutekelezwa chini ya ubora, kutokamilika, matumizi mabaya ya fedha za umma na udanganyifu.

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo tarehe 14 Oktoba, 2019 katika sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Baba waTaifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Wiki ya Vijana zilizofanyika Kitaifa katika uwanja wa Ilulu Mjini Lindi.

Rais Magufuli amekabidhi kitabu cha taarifa ya miradi hiyo kilichowasilishwa kwake na Kiongozi wa Mbio za Mwenge mwaka huu Mzee Mkongea Alikwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brig. Jen. John Mbungo nakumuagiza wote wakaobainika kuhusika katika dosari za miradi hiyo kufikishwa Mahakamani ili sheria zi chukue mkondo wake.


Katika taarifa hiyo Mzee Mkongea Ali amesema udanganyifu mkubwa umebaini kakatika miradi ya maji na amesisitiza kuwa endapo fedha nyingi zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kutatua tatizo la maji zitasimamiwa vizuri, tatizo hilo litapata ufumbuzi.

Amebainisha kuwa yeye na wakimbiza Mwenge wa Uhuru wenzake wamebaini kazi kubwa inayofanywa na Serikali ikiwemo miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini, kuongezeka kwani dhamu katika utumishi wa umma na kujengwa kwa miundombinu muhimu ya kuvutia uwekezaji mambo ambayo ni muhimu kwa maendeleo.

Kabla Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa hajasoma risala ya wananchi wa Tanzania, Waziri waNchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira naWenye Ulemavu Jenister Mhagama amesema mwaka huu Mwenge wa Uhuru umekimbizwa kwa miezi 7 katika jumla ya kilometa 26,274 ambapo umeweka mawe ya msingi, kufungua na kuzindua miradi ya maendeleo 1,390 yenye thamani ya shilingi Trilioni 4 na Bilioni 750 iliyopo katika Mikoa 31 na Halmashauri 195.

Kuhusu kumbukumbu ya Baba waTaifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Rais Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kumuenzi kwakutekeleza kwavitendo misingi yaUhuru naAzimio la Arusha ambalo linahimiza watu kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa, elimu kwa wote hasa elimu ya ufundi, kupiga vita umasikini na ukosefu waajira, kujenga miundombinu, uzalendo na nidhamu kwa watumishi wa umma.

Ameahidi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itajitahidi kwa kadri iwezavyo kumuenzi Baba wa Taifa na ametaja baadhi ya juhudi zilizofanywa kwa vitendo kuwa ni kupambana na rushwa ambapo Mahakama ya kushughulikia Ufisadi imeanzishwa, watumishi hewa takribani 20,000 na wafanyakazi wenye vyeti feki 14,000 wameondolewa katika utumishi wa umma, kutoa shilingi Bilioni 23.8 kwa ajili ya elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari, kutoa shilingiBilioni 470 kwa mwaka kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu, kuboresha huduma za afya ambapo hospitali mpya 69 na vituo vya afya 352 vinajengwa nakuongeza bajeti ya dawa kutoka shilingi Bilioni 31 hadi kufikia shilingi Bilioni 270.

Maeneo mengine ni kuboresha upatikanaji wahuduma zamaji Mijini naVijijini ambapo takribani shilingi Trilioni 2 zinatumika, kuhimiza ujenzi wa viwanda ambapo viwanda takribani 4,000 vimejengwa, kuanza ujenzi wa mradi mkubwa wa ujenzi wa Bwawa la Mwl. Nyerere litakalozalisha megawatti 2,115 za umeme ambapo shilingi Trilioni 6.5 zinatumika, kujenga reli ya kisasa (standard gauge railway – SGR) ambapo shilingi Trilioni 7.3 zinatumika, kujenga viwanja vya ndege 11, kununua ndege 11, kupanua bandari ambapo takribani shilingi Trilioni1 zinatumika, kununua meli mpya na kukarabati za zamani.

Aidha, Rais Magufuli amesema Serikali ya Awamu ya Tano inamuenzi Baba wa Taifa kwa kuhakikisha inasimamia vizuri rasilimali na mali asili zikiwemo misitu, wanyamapori na madini kupitia sheria mpya ya mwaka 2017 ambayo imewezesha kuongezeka kwa mapato ya madini kutoka shilingi Bilioni 191 mwaka 2016/17 hadi kufikia shilingi Bilioni 335 mwaka 2018/19, kuanzisha Hifadhi zaTaifa 4 ikiwemo Hifadhi yaTaifa ya Nyerere baada ya kumega Pori la Akiba la Selous na kuimarisha sekta ya Kilimo.

Kuhusu vijana, Rais Magufuli ameipongeza Serikali ya Awamu ya Nne iliyoongozwa na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete kwakurejesha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa vijana na ameahidi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendeleza mafunzo hayo.

Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Mawaziri wa Tanzania Bara na Zanzibar, Mabalozi, Wakuu wa Mikoa na viongozi wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.