Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Rais Samia Anawapenda Watu wenye Ulemavu - Mhe. Lulida


RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan amepongezwa kwa namna anavyoonesha upendo mkubwa kwa watu wenye ulemavu ikiwamo kupatiwa vitalu vya kuchimba dhahabu Mbogwe mkoani Geita.

Mbunge wa Kuteuliwa ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Riziki Lulida ameyasema hayo Aprili 4, 2023 bungeni alipokuwa akichangia mjadala wa azimio la Bunge la kumpongeza Mhe.Rais Samia kwa kuimarisha demokrasia nchini na kukuza diplomasia ya uchumi.

Amesema mwamko alionao Rais kwa watu wenye ulemavu umewafanya Mawaziri kuiga na kuwapenda watu wenye ulemavu ambapo kupitia Shirika la Madini (Stamico) wamepewa vitalu vya kuchimba dhahabu Mbogwe.

"Mimi mwenyewe nimekwenda pale kukaga vifaa kwa watu wenye ulemavu, wenye usikivu hafifu leo walemavu wanachimba dhahabu, nitanyamaza vipi kumpongeza Rais kwa hili, na napongeza Wizara ya kilimo wao wametoa hekari 50 kwa baadhi ya Wilaya kwa ajili ya watu wenye ulemavu sasa wenye ulemavu wa ngozi wataanza kulima, mfano Wilaya ya Chamwino wametoa hizo hekari na Wakala wa Mbegu ASA wanatoa mbegu,"amesema.

Amesisitiza kasi ya Rais kwa watu wenye ulemavu inaonesha katika kujenga uchumi jumuishi na dunia inatambua upendo huo.

"Watu wenye ulemavu kwasasa wanasikika na kueleweka,maeneo ambayo Rais ameonesha upendo alikula chakula na watu wenye ulemavu Ikulu, alituletea Sh.Milioni 150 watu wenye ulemavu katika mpira wa miguu kwa wenye ulemavu."

"Kupitia michezo vijana 12 wenye ulemavu wamepata ajira nje ya nchi wanashukuru sana familia zao zinanufaika," amesema.