Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Rais Samia aridhia watumishi waliondolewa kazini kwa kughushi vyeti kurejeshewa michango


RAIS SAMIA ARIDHIA WATUMISHI WALIONDOLEWA KAZINI KWA KUGHUSHI VYETI KUREJESHEWA MICHANGO YAO.

* Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ametoa Leo tarehe 26 Oktoba,2022 ametoa TAMKO kwa kubainisha yafuatayo:-

#Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameridhia kuwa watumishi walioondolewa kazini kwa sababu ya kugushi vyeti warudishiwe michango yao tu ambayo walichangia kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

#Kinachorejeshwa ni asilimia 5 kwa Watumishi ambao michango yao ilikatwa kwenye mshahara yao kwenda PSSSF na asilimia 10 kwa watumishi waliokuwa wanakatwa kupitia NSSF ambapo mifuko hiyo itafanya marejesho ambayo hayatahusisha michango iliyokuwa inawasilishwa na mwajiri wala malipo mengine yoyote ya ziada.

#Marejesho ya michango kwa watumishi hao yataanza kufanyika kuanzia Novemba 01, 2022, tunapenda jambo hili likamilike kwa muda mfupi.

#Ili kuwezesha malipo hayo kufanyika, mtumishi husika atatakiwa kwenda kwa aliyekuwa mwajiri wake akiwa na nyaraka zifuatazo: 'Passport size' mbili, taarifa za kibenki za akaunti iliyo hai, kitambulisho cha Taifa au mpiga kura au leseni ya udereva.

#Mtumishi atatakiwa kujaza na kusaini hati ya ridhaa kwa aliyekuwa mwajiri wake na waajiri watawajibika kuwasilisha kwenye mifuko hati za ridhaa pamoja na nyaraka nyingine, hakutakuwa na mawasiliano ya moja kwa moja kati ya watumishi na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

#Natoa rai kwa waajiri kuhakikisha kwamba wanawapa ushirikiano watumishi husika kwa kukamilisha na kuwasilisha mara moja nyaraka zinazotakiwa na Mifuko ya Jamii, nawasihi msikae na nyaraka za watumishi ili kazi hii ifanyike ndani ya muda mfupi.

#Tungependa kuona kwamba maelekezo yaliyotolewa na Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan yanafanyiwa kazi ndani ya muda mfupi, tunaamini kwamba mkitoa ushirikiano haitapita miezi miwili zoezi hili litakuwa limekamilika.