Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Rais Samia: Uwekezaji wa rasilimali Watu kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa Vijana


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema uwekezaji wa rasilimali watu hususani kwa vijana kutawezesha kuongeza tija na ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi katika bara la Afrika.

Amesema hayo Julai 26, 2023 wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Saalam.

Sambamba na hayo, amesema yapo malengo na ajenda za maendeleo ya Afrika na baadhi ya malengo hayo ni pamoja na mafanikio ya ukuaji jumuishi wa uchumi na maendeleo endelevu, pia Afrika yenye utengamano wa kisiasa.

Vilevile, mwelekeo wa kimapinduzi kuwa na Afrika inayozingatia misingi ya Utawala Bora, Demokrasia, Haki za binadamu na utawala wa sheria, halikadhalika Afrika itakayo pata maendeleo yake kwa kuzingatia vipaji hususani vya wanawake na vijana.

Aidha, Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo inadhamana ya kusimamia na kuratibu masuala ya Vijana kupitia Idara ya Maendeleo ya vijana imeendelea kutengeneza mazingira wezeshi kwa vijana ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo ya taifa.