News
Ridhiwani: Serikali inatoa kipaumbele cha Ajira kwa Wenye Ulemavu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatoa kipaumbele kwa Watu wenye Ulemavu kupata Ajira.
Amesema kwa kutambua mchango wa Watu wenye Ulemavu katika kukuza Taifa hili, serikali imeweka mikakati ya kuwawezesha kujiajiri kwa kutenga mikopo maalum ili iwasaidie kuinua Uchumi wao.
Mhe. Ridhiwani amebainisha hayo Jijini Dar es salaam kupitia Clouds FM, ambapo amesema serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea kuratibu masuala ya Ajira kuwasaidia vijana kuondokana na changamoto za Ajira.