News
Sangu amshukuru Rais Samia kwa maendeleo jimbo ka Kwela
Mbunge wa Jimbo la Kwela na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Clement Sangu, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuleta maendeleo wananchi wa Jimbo la Kwera, mkoani Rukwa, huku akiwataka wananchi kuendelea kuthamini jitihada zinazofanywa na Serikali.
Sangu ametoa shukrani hizo wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika Jimbo la Kwera, Mhe. Sangu ambapo amewakaribisha wakimbiza Mwenge na kueleza kuwa wananchi wa eneo hilo wanathamini juhudi za Serikali katika kuboresha maisha yao kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha, Mhe. Sangu amewahimiza wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuleta maendeleo na kudumisha mshikamano wa Taifa.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2026, Wazo Michael Mwang’onda amewapongeza wananchi wa Laela kwa kuupokea Mwenge kwa heshima kubwa, kuanzia mapokezi hadi katika viwanja vya mkesha, akieleza kuwa wameonesha uzalendo na kuthamini Mwenge wa Uhuru.
Amesema Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 zitahitimishwa katika eneo la Sumbawanga Mjini, hivyo kuwataka wananchi kuendelea kuenzi tunu za Taifa na kushiriki kikamilifu katika kulinda amani na mshikamano wa Watanzania.
Vilevile, amewahimiza wananchi kuwa mabalozi wa amani kwa wenzao, akisisitiza kuwa kila Mtanzania ana wajibu wa kulinda utulivu na kuimarisha umoja wa kitaifa ili kuweka mazingira bora ya maendeleo endelevu nchini.


