Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Serikali haito wavumilia waajiri wasio wasilisha michango NSSF - Ndejembi


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe Deogratius Ndejembi amesema serikali haitawavumilia waajiri wa sekta binafsi ambao wanakata michango ya wafanyakazi wao bila kuiwasilisha katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Mhe Ndejembi ametoa onyo hilo wakati alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za NSSF jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya ya taasisi hiyo.

Amesema ni kosa kisheria kwa muajiri kutowasilisha michango ya mfanyakazi wake NSSF na hivyo kuwanyima haki wafanyakazi wao ambao wanashindwa kulipwa mafao yao kwa wakati pindi wanapostaafu.

“ Niwatake waajiri wote kutimiza takwa hili la kisheria la kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao NSSF. Na wale wenye tabia ya kutowasilisha niwatake waache mara moja tabia kwa sababu Serikali hii ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan haitofumbia macho muajiri atakayejaribu kuzuia haki ya mfanyakazi wake.

Hatutomvumilia muajiri yeyote mwenye tabia hizo na yeyote ambaye atabainika tutamchukulia hatua za kisheria,” Amesema Mhe Ndejembi.

Katika ziara hiyo Mhe Waziri Ndejembi aliambatana na Kamishna wa Kazi, Bi Suzan Mkangwa.