Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Serikali kuendelea kushirikiana na Asasi za Kiraia katika kutatua changamoto za vijana


Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imeendelea kushirikiana na Asasi za kiraia nchini zinazoshughulikia masuala ya vijana kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi ameeleza hayo wakati wa uzinduzi wa Kongamani la Vijana Tanzani (Tanzania Youth Forum) lililofanyika, Dar es Salaam Agosti 9, 2022 kuelekea katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani, Agosti 12, 2022.

Ameleza kuwa, dhamira ya Serikali ni kuendelea kushirikisha vijana katika nyanja mbalimbali, sambamba na kufungua fursa zaidi za ajira, mitaji Pamoja na kuwatengeneza mazingira wezeshi na jumuishi yatakayowasaidia kushiriki kikamilifu kwenye nafasi za Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii.

Ameongeza kuwa, Serikali kwa kutambua umuhimu wa vijana imechukua hatua za kuwashirikisha kwenye sekta tofauti kwa ajili ya mustakabili wa taifa,

Akibainisha hatua hizo Kwa kuzitaja kuwa ni; kuwekeza zaidi katika sekta ya Elimu iliyo bora kwa kuweka Sera ya elimu bila Ada kuanzia elimu ya awali, msingi na Sekondari,

Mhe. Katambi amesema wameongeza Bajeti ya mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu kutoka shilingi Billioni 367.35 mwaka 2015 hadi kufikia shilingi Billioni 570 kwa mwaka 2021/22.

Amesisitiza kuwa kupitia Programu ya kukuza Ujuzi kwa vijana 28,941 wamekwishapatiwa mafunzo ya Uanagenzi katika fani za ufundi zikiwemo ushonaji nguo, useremala, uashi, uchongaji wa vipuri, umeme, upishi na huduma za Hoteli.

Mhe. Katambi amefafanua kuwa Vijana 20,432 wametambuliwa na kurasimisha ujuzi wao uliopatikana nje ya Mfumo rasmi wa shule,

Vijana 5,975 wahitimu wa elimu ya juu wa wamewezeshwa kupata mafunzo ya uzoefu kazini (Internship) kwenye viwanda, Taasisi na Makampuni kutoka sekta binafsi na sekta ya umma nchini.

Pia elimu ya kilimo cha kisasa kinachotumia teknolojia ya Kitalunyumba imetolewa kwa vijana 8,980 katika Mikoa 12 katika awamu ya kwanza.

Vijana wamewezeshwa kiuchumi kwa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana pamoja na fedha zinazotengwa na Halmashauri nchini.