Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Serikali ya Awamu ya Sita inawajali na kuwathamini Watu wenye Ulemavu: Mhe. Katambi


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwajali na kuwathamini Watu wenye Ulemavu kwa kuhakikisha inakuza ustawi wa kundi hilo.

Mhe. Katambi amesema hayo leo Juni 19, 2023 alipokutana na wageni wake kutoka Chama cha Wazazi wa Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBAHT), katika viwanja vya Bunge, jijini Dodoma.

Aidha, amesema kuwa Serikali imeboresha huduma kwa Watu Wenye Ulemavu ambapo mwaka 2022/2023 ilitenga jumla ya shilingi bilioni 3.46 kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa vyuo vya Watu Wenye Ulemavu vya Mtapika (Masasi – Mtwara), Luanzari (Tabora), Sabasaba (Singida) na Yombo (Dar es Salaam).

Vile vile, Naibu Waziri Katambi amesema kuwa Serikali katika mwaka 2023/2024 imepanga kuwawezesha Watu wenye Ulemavu kujiajiri na kuajiriwa kwa kuongeza fursa za mafunzo ya ufundi stadi na marekebisho.

Kwa upande mwengine Mhe. Katambi amesema Serikali imetengeneza Mfumo wa Kielektroniki wa Watu Wenye Ulemavu ili kuongeza ufanisi wa upatikanaji wa taarifa za watu wenye ulemavu. Mfumo huo utawezesha kumtambua mtu mmoja mmoja mwenye ulemavu, mahali alipo, shughuli anayoifanya na mahitaji yake.