Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

SINGIDA YAENDELEA KUNUFAIKA NA PROGRAMU YA UKUZAJI UJUZI. Na; OWM - KVAU, Singida Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi,Vijana,Ajira na Watu Wenye Ulemavu imeendelea kutoa mafunzo kwa vitendo ya ukuz


Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi,Vijana,Ajira na Watu Wenye Ulemavu imeendelea kutoa mafunzo kwa vitendo ya ukuzaji ujuzi kwa wakulima na wasindikaji wadogo wa zao la alizeti ili kuwawezesha kuongeza tija wa bidhaa wanazozalisha .

Mafunzo hayo yamefanyika katika chuo cha Maeneo ya Jamii (FDC) Singida Leo Novemba 11 ,2025 Ikiwa ni utekelezaji wa Programu ya Taifa ya kukuza Ujuzi inayoratibiwa na ofisi hiyo ikishirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI).

Akizungumza kwenye mafunzo hayo Bw.Genes Swai, Mchumi kutoka Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi amesema mafunzo hayo yanalenga kuongeza ufanisi na tija, kuongeza mapato na maendeleo ya kiuchumi, kufanikisha ujasiriamali ujuzi pamoja na kuwajengea uwezo wa kibiashara.

Kwa ipande wao washiriki wa mafunzo akiwemo Neema Mbura kutoka Singida ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yamewasaidia kufahamu mbinu za uongezaji thamani wa zao hilo na kuahidi kuongeza shamba na kuzingatia kanuni bora za kilimo ili kupata tija na kukuza kipato.