Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Tanzania, Austria kushirikiana katika Ajira


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imekubaliana kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Austria juu ya kufungua fursa za ajira kwa watanzania nchini humo.

Ajira hizo zitawahusisha watanzania wenye ujuzi na ambao hawana na kuwaongezea ujuzi katika sekta ya kilimo, viwanda na biashara.

Makubaliano hayo yamefikiwa leo katika Mkutano wa Naibu Waziri Ofisi hiyo Mhe. Patrobas Katambi na Waziri wa Kazi na Uchumi Austria Prof. Martin Kocher leo Oktoba 25, 2023 Jijini Dar es salaam.

Mhe. Katambi amesema wamekubaliana kujifunza namna ambavyo wanaendesha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na elimu ya ufundi ambapo hadi sasa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyuo hivyo nchi nzima.

“Austria wana uzoefu, ujuzi na ubobevu katika masuala ya kiuchumi, ajira na elimu hivyo tunataka kutumia nafasi hiyo kufungua fursa kwa vijana wa kitanzania kujifunza namna ambavyo wenzetu wanafanya” amesem