Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Tanzania kuendelea kushirikiana na Kenya - Mhe. Katambi


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi ameihakikishia serikali ya Kenya kupitia Wizara ya Kazi ya nchi hiyo kuwa wataendelea kushirikiana katika masuala ya kazi na ajira.

Mhe. Katambi amebainisha kuwa Ofisi hiyo inaratibu masuala yote ya kazi na Ajira na kuhakikisha inaondoa ubaguzi katika fursa za Ajira na Kazi.

Amebainisha hayo, Aprili 20, 2023 Jijini Dodoma, baada ya Kukutana na ujumbe wa Wizara ya Kazi nchini Kenya uliofika nchini kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa namna nchi hizo zinavyoratibu masuala ya kazi.

Mhe. Katambi amesisitiza kuwa Ofisi hiyo inalo jukumu la kukuza ujuzi kwa vijana ambapo serikali inatenga bajeti ili kuwasaidia vijana wanapomaliza masomo yao waweze kujiajiri ama kuajiriwa.

Kiongozi wa ujumbe huo, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Hifadhi ya Jamii nchini Kenya, Mhe. Geofrey Kaituko ameipongeza Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa namna ambavyo inaratibu vizuri jaira za nje ya nchi kupitia Kitengo cha Huduma za Ajira.

Mhe. Kaituko amesema ziara hiyo nchini Tanzania imewasaidia kujifunza namna ambavyo Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo zinavyofanya kazi ikiwemo Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Wtumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).