Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

​Tunawashirikisha Vijana Kiuchumi: Mhe. Katambi


Serikali imeendelea kuwashirikisha vijana katika mipango na programu za kiuchumi ili wajiajiri na kuajiri wenzao.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi ameyasema hayo alipokuwa akikagua maendeleo ya utekelezaji wa Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) kwenye kituo atamizi cha vijana kilichopo Chuo cha Mafunzo ya Kilimo (KATC), mkoani Kilimanjaro.

Mhe. Katambi amesema serikali imewajengea mifumo mizuri vijana inayowasaidia kupata mitaji ya kuanzisha shughuli za kiuchumi na kuwaasa wanufaika wa BBT kuwa mabalozi wa kilimo biashara nchini ili kukuza uchumi na maendeleo ya nchi Taifa.

Aidha, amesema kuwa utekelezaji wa mradi wa BBT ni dhamira ya serikali chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha vijana wanapata fursa katika sekta za kiuchumi ikiwamo madini, kilimo, mifugo na uvuvi.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kisare Makori amewataka vijana kuchangamkia fursa zilizopo katika mradi huo ili waweze kujikwamua kiuchumi, huku Mnufaika wa BBT, Bw. Orest Kibiki wakimshukuru Rais Samia kwa kutoa kipaumbele kwenye masuala ya vijana.