Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Vijana 121,898 Wanufaika na Programu ya Ukuzaji Ujuzi


WAZIRI Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema vijana 121,898 wamepata mafunzo kupitia Programu ya Ukuzaji Ujuzi kwa kipindi cha 2017 hadi 2023.

Akitoa hotuba ya kuahirisha mkutano 13 wa bunge Novemba 10, 2023, Mhe.Majaliwa amesema kupitia programu hiyo vijana 91,106 wamepata ujuzi kwa njia ya uanagenzi, 22,296 wamerasimishiwa ujuzi uliopatikana katika mfumo usio rasmi.

“Vijana 6,300 wamepata mafunzo ya uzoefu kazini na vijana 2,196 waliokuwa kazini wameongezewa ujuzi, kupitia Mpango wa Jenga Kesho iliyobora vijana 812 wamedahiliwa na wanashiriki mafunzo ya Kilimo Biashara,”

Aidha, amesema katika mwaka wa fedha 2022/23 serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana imetoa mikopo ya sh. bilioni 1.88 kwa miradi 85 yenye vijana 595 na mwaka 2023/24 serikali imeendelea kutoa mikopo na hadi kufikia Oktoba 2023 sh.bilioni 1.27 zimetolewa kwa miradi 56 yenye vijana 392,” amesema